Ndugu wafukua maiti iliyozikwa miezi 3

01Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
MBEYA
Nipashe
Ndugu wafukua maiti iliyozikwa miezi 3

Ndugu wa Marehemu Tulizo Konga wa Kijiji cha Igumbilo Kata ya Chimala mkoani Mbeya, wamefukua kaburi la ndugu yao mara baada ya kupata kibali kutoka kwa mamlaka za kisheria ili kupata uhakika wa chanzo cha kifo cha ndugu yao, aliyefariki Dunia Machi 25 na kuzikwa Machi 28.

Mwili wa Marehemu Tulizo Konga, ukifukuliwa huko mkoani Mbeya.

Ndugu wamedai kuwa mara baada ya kutilia mashaka namna kifo cha ndugu yao kilivyotokea, ndiyo maana waliamua kufuatilia hatua zote lengo likiwa ni kuujua ukweli kama ndugu yao alifariki kifo cha kawaida ama aliuawa, kutokana na mazingira ya kifo hicho kuwa ni ya mashaka.

Wameendelea kudai kuwa hata taarifa za kifo cha Tulizo, walizipata kutoka kwa majirani baada ya mume wake Kelvin Mwanjemba kuwa kimya, huku akidai mkewe alifariki akiwa Hospitali ya Chimala, wakati Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo akidai alimpokea mwili wa Tulizo na si mgonjwa.

Mara baada ya mwili huo kufukuliwa ulipelekwa katika Hospitali ya Chimala kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi na baada ya madaktari kuchukua vipimo, mwili huo ulizikwa tena kwa mara nyingine usiku wa kuamkia leo Julai 1, 2020.

Chanzo: https://www.eatv.tv/

Habari Kubwa