Neema kuwashukia wastaafu wanaodai mafao Psssf

16Apr 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Neema kuwashukia wastaafu wanaodai mafao Psssf

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama amesema juzi serikali imetoa Sh.Bilioni 100 kwa ajili ya kuwalipa wastaafu 6,793 wa Mfuko wa Jamii wa Watumishi wa Umma(PSSSF).

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama.

Ufafanuzi huo aliutoa leo bungeni, kufuatia mchango uliotolewa na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Halima Mdee kudai kuwa serikali inadaiwa fedha nyingi na wastaafu nchini.

Mdee alitaka serikali kulipa deni inalodaiwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili iweze kuwa endelevu na wastaafu walipwe kwa wakati.

“Hili ni donda ndugu zito kabisa ni upande wa serikali fedha inazokopa inazotakiwa kulipa kwa riba na kudhamini taasisi zake, fedha hazilipwi, mwaka 2018 tuliunganisha mifuko tukaambiwa ili ufanisi uwe bora zaidi lakini Hotuba ya Waziri Mkuu imesema tumepunguza gharama za uendeshaji, lakini usugu upo kwa zile fedha mlizokopa mnakigugumizi gani kulipa,”amesema.

Aidha, amesema katika Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa fedha za serikali (CAG), madeni ya ndani ambayo serikali inadaiwa ni Sh.Trilioni 2.7 lakini kuna fedha zingine Sh.Trilioni 7.1 ambazo PSSSF ilipewa jukumu la kulipa wastaafu ambao wamekidhi vigezo vya kulipwa lakini hawajachangiwa.

Habari Kubwa