Neema waathirika mafuriko

23Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Neema waathirika mafuriko

Watu walioathiriwa na mafuriko hayo yaliyotokana na mvua katika kata 11 za vijiji 16 wilayani humo, wameanza kugawiwa viwanja kwa ajili ya makazi mapya katika maeneo mengine wilayani humo.

Mjumbe wa Halmashauri kuu wa Mkoa wa Morogoro ya CCM kutoka wilaya ya Kilosa,Jonas Nkya, akimsikiliza mmoja wa mama ALIYOATHIRIKA na mafuriko katika kata ya Tindiga.

Aliyetangaza neema hiyo kwa waathirika ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilosa, Kessy Mkambala.

Akizungumza wakati akipokea misaada wa vyakula, maji na sabuni kutoka kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilosa, Jonas Nkya, Mkambala, alisema kwa kuanzia Halmashauri yake itapima viwanja 2,500 kwa ajili ya makazi mapya ya waathirika hao. Kwa mujibu wa Mkambala, viwanja hivyo vitapimwa katika maeneo mbalimbali na wameanza kuvigawa kwa waathirika katika Kata ya Tindiga ambao nyumba zao zimebomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa baada ya hapo watavigawa kwa wakazi ambao nyumba zao zimepata nyufa na kumaliziwa na wenye maeneo hayo yaliyochukuliwa na Serikali. 

Habari Kubwa