Nitatuma timu ya ukaguzi mradi wa maji wilayani Kiroka - DC Msulwa

18Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Morogoro
Nipashe Jumapili
Nitatuma timu ya ukaguzi mradi wa maji wilayani Kiroka - DC Msulwa

​​​​​​​MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa, amesema atatuma timu ya ukaguzi kwenye mradi wa maji Kiroka na miradi mingine wilayani humo kwa lengo la kubaini ukusanyaji na matumizi ya fedha za maji zinazo kusanywa kutoka kwa wateja.

​​​​​​​Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa.

DC Msulwa amesema hayo baada ya kikao kifupi kilichohudhuriwa na  baadhi ya watumishi wa Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira pamoja viongozi wa Kata ya Kiroka.

Msulwa amewataka Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira katika Wilaya hiyo kuhakikisha wanatoa elimu kwa kamati za jumuiya ya watumiaji wa maji kwa lengo la kuongeza wigo wa utunzaji wa miundombinu ya maji.

Naye Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira, Mhandisi Grace Lymo, amesema kwa sasa serikali imepanga kukarabati mradi wa maji katika Kata hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Habari Kubwa