Nondo atangaza nia kugombea Kigoma Mjini

05Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Nondo atangaza nia kugombea Kigoma Mjini

MWENYEKITI wa Ngome ya Vijana wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Abdul Nondo, ametangaza nia ya kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Mjini.

Abdul Nondo.

Nondo amesema hayo leo Julai 5, Mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari, huku akisema lengo la kutaka kimiliki Jimbo hilo ni kuongeza na kuchochea shughuli za kimaendeleo na mzunguko wa kifedha katika Jimbo hulo.

Nondo amezitaja hatua tano za demokrasia ya uchaguzi kuwa ni pamoja na kutangaza nia, kuchukua na kurejesha fomu ni hatua ya pili ya demokrasia kwa mwanasiasa na hatua ya tatu ni kupitishwa au kutopitishwa na vikao vya chama (kura za maoni), hatua ya nne ni kuingia ulingoni kupeperusha bendera ya chama  baada ya kuteuliwa na vikao vya chama huku atua ya tano ni kuingia Bungeni baada ya kupewa ridhaa na wananchi.

Mbali na hayo, Nondo amesema Chama hicho kinaamini katika misingi 10 huku msingi wa saba ni msingi wa Demokrasia kama vile kuwa huru kuchagua na kuchaguliwa , hivyo kwa namna hiyo chama ndio kinaamua nani wa kupeperusha bendera ya chama hicho hasa katika Jimbo hilo.

Nondo amesema ikiwa kama atateuliwa na chama chake atahakikisha anaondoa changamoto zilizopo katika Jimbo hilo ambapo ni pamoja na Jimbo hilo kutokuwa na mzunguko wa kifedha kutokana na uchache  wa shughuli za kiuchumi

Aidha, Nondo amesema baada ya kazi na majukumu makubwa aliyoyafanya Zitto Kabwe katika kipindi chake cha miaka 5 ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kogoma Mjini, lakini bado wananchi hao wana fursa ya kuendelea kuchagua Mbunge mwenye uwezo na ujasiri wa kuisimamia, kuikosoa na kuishauri serikali kikamilifu kwa maslahi ya wananchi.

Habari Kubwa