Norway yaitaja Tanzania kama kielelezo cha amani mchakato kampeni

21Sep 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SAALAM
Nipashe
Norway yaitaja Tanzania kama kielelezo cha amani mchakato kampeni

Tanzania imetajwa kama Nchi ya kielelezo cha amani na Demokrasia katika Bara la Afrika utokana na mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu unavyofanyika kwa amani,utulivu na usawa kwa wagombea wa vyama vyote huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Kabudi akimuonesha Balozi Norway nchini, Elisabeth Jacobsen moja ya kipengele cha sheria ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi wakati alipokuwa akimkabidhi nakala ya nyaraka hizo.

Balozi wa Norway nchini Tanzania Balozi Elisabeth Jacobsen ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi na kuongeza kuwa maandalizi ya uchaguzi mkuu yamefanyika kwa kufuata taratibu za kisheria huku tume ya Taifa ya Uchaguzi ikishughulikia baadhi ya malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya vyama vya siasa na wadau mbalimbali jambo ambalo linaifanya Tanzania kuwa kinara wa demokrasia katika mchakato mzima wa uchaguzi.

 Pamoja na masuala ya kisiasa Balozi huyo amesema katika mazungumzo yao wamegusia pia masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi hususani katika suala la elimu,afya,nishati na uwekezaji pamoja na biashara baina ya nchi hizo mbili.

 

 

Habari Kubwa