Nyalandu: Siwezi kuondoka Chadema, nampenda Tundu Lissu

04Aug 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
Nyalandu: Siwezi kuondoka Chadema, nampenda Tundu Lissu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu amesema kuwa hawezi kuondoka Chadema baada ya kushindwa kura za maoni na kwamba anampenda mshindi wa kura hizo Tundu Lissu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu akiwa na mshindi wa nafasi ya ugombea urais bara, Tundu Lissu.

Akizungumza baada ya upigaji wa kura za maoni kupitia chama hicho ili kupata mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho jana katika ukumbi wa Mlimani City, Nyalandu alisema kuwa alishiriki kutafuta ndege iliyotumika kumsafirisha kwenda Nairobi kutibiwa baada ya tukio la kupigwa risasi Jijini Dodoma Septemba mwaka 2017 na kwamba aliumizwa sana na tukio lile na hivyo kutokana na upendo huo hawezi kuisaliti Chadema.

"Nimeyapokea matokeo haya sio kama adhabu kwa Nyalandu bali ni mapenzi yaliyotukuka mapenzi makubwa kwa Mheshimiwa Lissu, Lissu ambaye mimi hapa ninampenda sana huu ni wakati wa Tundu  Lissu "- amesema Nyalandu.

 

Habari Kubwa