Ofisa mifugo mbaroni kumkashifu Naibu Waziri Katambi

19Jul 2021
Marco Maduhu
SHINYANGA
Nipashe
Ofisa mifugo mbaroni kumkashifu Naibu Waziri Katambi

OFISA Mifugo Manispaa ya Shinyanga, Velan Mwalukwa, ametiwa mbaroni kwa kumtolea lugha chafu Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira.

Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, akizungumza wananchi wa Ibinzamata na kuwaeleza mikakati yake ya kuwaletea maendeleo na kutatua kero zao.

Mwalukwa, ametiwa Mbaroni jana wakati wa mkutano wa Mbunge Katambi, Kata ya Ibinzamata alipoitwa kujibu tuhuma zinazo mkabili, za kudaiwa kuhozi ardhi ya Mwananchi Zacharia Tingwa mkazi wa kata hiyo, na kutoa lugha zisizo za staha kwa mbunge huyo.

Kabla ya kuanza kujibu tuhuma hizo, Mwalukwa alianza kumtolea lugha chafu na za kumkejeli mbunge huyo, hali ambayo ili mkasilisha Katambi na kuagiza awekwe chini ya ulinzi kwa utovu wa nidhamu, na kisha baadae akachukuliwa na Polisi.

Aidha Katambi akizungumzia tukio hilo, alisema amesikitishwa na mtumishi huyo wa umma, kumdharau Mbunge tena Naibu Waziri mbele ya wananchi, na hivyo kuamua kumchukulia hatua, ili liwe fundisho kwa wengine.

Wananchi wa Ibinzamata wakiwe kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

"Huyu mtu anaonekana ana dharau na jeuri, mimi ana nifanyia hivi je Mwananchi wa kawaida, na hasa huyu ambaye  ana mgogoro naye, si ndiyo balaa kabisa, hebu ngoja tumtia adabu ili tuone jeuri yake ipo wapi," alisema Katambi.

"Suala hili la Mgogoro baina yake na huyu Mwananchi, nitalivalia njuga Tena bahati nzuri na Mimi ni Mwanasheria, na sita pendelea upande wowote ule, mwenye haki na hilo eneo atapata haki yake," aliongeza.

Katika hatua nyingine Katambi, aliwahidi wananchi wa Ibinzamata kuwa ataendelea kutatua changamoto ambazo zinawakabili, ikiwamo Sekta ya Afya, Elimu, ujenzi wa Barabara, pamoja na kushughulia malipo ya Wastaafu kutoka chama cha ushirika mkoani Shinyanga SHIRECU.

Awali Mwanchi huyo Zacharia Tingwa, akitoa malalamiko yake ya kudhurumiwa ardhi, alidai kuwa eneo hilo ni lake, lakini Ofisa huyo Mifugo amekuwa akitumia Pesa ili amnyang'anye na kufikia hatua ya kuweka familia yake yote rumande na kumtolea vitisho.

Habari Kubwa