OIKOS EA yawapa 'tochi' wananchi kufukuzia wanyama wakali

17Jun 2019
Zanura Mollel
LONGIDO
Nipashe
OIKOS EA yawapa 'tochi' wananchi kufukuzia wanyama wakali

SHIRIKA la Maendeleo ya jamii OIKOS EA, linalofanya kazi katika Wilaya ya Longido chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) limekabidhi kurunzi (tochi) maalumu kwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Enduiment (EWMA) kwa ajili ya kufukuzia wanyama wakali maeneo ya kilimo na ufugaji.

Meneja Wa EWMA Peter Millanga akizungumza na walengwa Wa kurunzi hizo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mratibu wa mradi wa kudhibiti migongano baina ya wanyama na binadamu kutoka OIKOS EA (HWC), Pascal Simon amesema lengo hasa la kutoa kurunzi hizo ni kwa ajili ya kuondoa migogoro baina ya wanyama, mifugo na binadamu ndani ya hifadhi ya (EWMA).

Ameeleza kuwa kurunzi hizo ni michango ya wananchi 18 ambao walichanga fedha nusu na shirika nalo likawaongezea, huku akidai kuwa kurunzi hizo zinauwezo wakukaa na moto (chanji) hadi masaa 48 kutokana na matumizi ya mtu binafsi.

Aina ya kurunzi iliyokabidhiwa kwa jumuiya kwenda kwa wanachi wa (EWMA)

"Tulikubaliana  wananchi wachangie asilimia 50 na shirika nalo asilimia 50,  kati ya wananchi 18 walio changa fedha hizo  kila mmoja alitoa sh   laki 168,750" ameeleza Simon

Amefafanua kuwa kurunzi hizo zilichelewa kuwafikia walengwa kwa wakati kutokana na shirika kuagiza nchini China huku kukiwa naongezeko la thamani kwa kodi pamoja na gharama za usafirishaji ,huku shirika hilo likiwa ni miongoni mwa (NGO's) zinazolipa kodi nchini.

"Tulivyoagiza kiwandani huko China ,walituambia hawawezi kutuma mzigo wabkurunzi 18 labda muagize kuanzia kurunzi 500, wannachi watusamehe kwa kuwacheleweshe si makosa yetu na hatukukusudia kuchelewesha" ameomba Pascal

Pascal simon Mratibu wa mradi wa HWC kutoa Shirika la Oikos Ea akionyesha kurunzi hilo kwa wananchi.

Hata hivyo alieleza kuwa kurunzi za awali walizokua wanategemea kuzipata zimekosekana na kufanikiwa kupata za aina nyingine ambayo kurunzi moja inayothamani ya sh laki 413000 huku zote 18 zikiwa na thamani ya sh million 721000

" kurunzi hizo ni aina ya Zartek(ZA _479) zina warrants ya mwaka mmoja ,tumekabidhi 17 ,wakati Wa kukagua kabla hatujazileta kwenu kurunzi moja ilionekana kuwa na tatizo hivyo tumeirejesha kwa ajili ya kubadilishwa na wiki ijayo itakua imeletwa na kukabidhiwa kwa mlengwa" alifafanua Pascal

Meneja Wa EWMA Peter Millanga aliwataka walengwa Wa kurunzi hizo kuzitumia kwa kile walicho elekezwa pamoja na kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika vita dhidi ya ujangili Wa wanyamapori.

Baadhi ya wakijiji waliopewa kurunzi hizo wakiwa wanasubiri kukabidhiwa kutoka kwa Meneja wa EWMA.

"Naomba tumieni kwa kile mlichoelekezwa ,ukimuazima jangili tutajua na tutakuchukulia hatua" alidai Millanga

Hata hivyo aliwata walengwa hao kuwa hamasisha vijana kujitokeza nyakati za usiku kufukuza wanyama wakali katika maeneo ya kilimo na Mifugo kwa kushirikiana na askari Wa jumuiya hivyo (EWMA) 

"Wanyama hawa ni kweli ni waharibifu kwa mazao na mifugo, tembo, mbogo ,pundamilia,lakini ni vyanzo vya mapato pia kwa jumuiya ,tukiwa na wanyama tutapata watalii wengi ndani ya hifadhi yetu ,japo kwa sasa jumuiya haina fidia kwa lolote linalofanywa na wanyama hawa,tusiwaue mambo yatakua mazuri bado jumuiya ni changa" alidai Millanga

Naye Ibrahim Simon mkazi Wa kata ya Olmolog amethibitisha kupokea kwa kurunzi hiyo akiwa miongoni mwa wananchi 18 wakiochanga fedha,na kuiomba jumuiya hivyo kuhakikisha wanakua na kurunzi za kutosha ili mwana jumuiya yeyote atakaye hitaji aweze kuipata kwa haraka

" Tunaomba jumuiya muwe na kurunzi hizo ili ziwasaidie wanajumuiya wasiojiweza kununua na hata wale wenye uwezo wachangie gharama na kupewa za kwao binafsi" ameomba

Vijiji vilivyopo kwenye jumuiya hiyo ni vijiji tisa ambavyo ni Ngereyani, Tingatinga,Sinya ,Elerai,Olmolog,Kitendeni,Kamwanga,Lerangwa na Irikaswa vyote vikiwa ndani ya tarafa ya Enduiment.

Habari Kubwa