Onyango apewa gari na Rais Museveni

07May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Onyango apewa gari na Rais Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven amempa zawadi ya gari aina Mitsubishi Pajero golikipa wa Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini na Timu ya Taifa ya Uganda Dennis Onyango (36).

Onyango amepewa zawadi hiyo kwa heshima ya kuitumikia timu ya Taifa ya Uganda kwa miaka 16 na hivi karibuni alitangaza kustaafu kuitumikia Uganda na sasa anabaki kuitumikia Mamelod Sundowns pekee.

Gari alilopewa Onyango na Rais Museveni linatajwa kuwa na thamani ya USD 52,490/= (Tsh Milioni 121.7).

Habari Kubwa