Onyo kali watakaotoa na kusambaza taarifa za uongo za Corona

18Mar 2020
Happy Severine
Bariadi
Nipashe
Onyo kali watakaotoa na kusambaza taarifa za uongo za Corona

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Festo Kiswaga ametoa onyo kwa wananchi wote watakaoendelea kutoa na kusambaza taarifa potofu juu ya  ugonjwa wa Corona kwani vyombo vya dola havitasita kuwachukulia hatua kali.

mchungaji wa kanisa la morovian Bariadi Martin Mketo (aliyesimama) akimkaribisha mkuu wa Wilaya ya BariadiFesto Kiswaga (kulia) azungumze na umoja wa wanafunzi wa kikristu wa vyuo vikuu Nchini(USCF) pindi alipofika katika kijiji cha Gamboshi kwa ajili ya kuzungumza nao.

Kiswaga amesema hayo leo wakati wa mazungumzo yake na umoja wa wanafunzi wa kikristu wa vyuo,yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Gamboshi Wilayani humo.

Amesema  wananchi wasikurupuke kwa kutoa na kusambaza taarifa za uongo kwani zipo mamlaka husika zinazohusika kutoa taarifa rasmi za serikali.

"Natoa onyo kali kwa wale wanatakao endele kutoa na kusambaza taarifa za uongo juu ya ugonjwa wa corona na atakayebainika anabainika kufanya hivyo sheria itachukua  mkondo wake" Kiswaga

Wanafunzi wa Umoja wa Kikristu wa Vyuo Vikuu (USCF) wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga (hayupo pichani)

Sambamba na hilo Kiswaga amezuia mikusanyiko ya harusi,mikutano ya watu wengi na watu kutokukumbatia ili kuepuka kuenea na kuambukizana ugonjwa huo.

Aidha amewataka viongozi wote wa serikali kuanzia ngazi za Tarafa,kata na vijiji kuwatangazia wananchi wao njia sahihi za kujikinga na ugonjwa wa corona.

Habari Kubwa