Orodha ya abiria waliokuwa kwenye ndege iliyopata ajali yatolewa

10Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Orodha ya abiria waliokuwa kwenye ndege iliyopata ajali yatolewa

Ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Ethiopia ambayo ilikuwa na watu 157, imeanguka muda mfupi baada ya kupaa, ambapo watu wote waliopo kwenye ndege hiyo wanahofiwa kupoteza maisha.

Habari zilizothibitishwa na Shirika la ndege la Ethiopia imesema kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitoka Ethiopia kwenda Nairobi, ilipata hitilafu angani na kupelekea kuanguka kwake.

Shirika limesema tayari imeshatuma timu yake eneo la tukio ili kuokoa majeruhi kama wapo, na muda si mrefu watatoa namba za abiria waliomo ili ndugu zao waweze kuwatambua.

Serikali ya nchi hiyo tayari imeagiza vyombo vya usalama kwenda eneo la tukio, na kufanya lolote liwezekanalo kunasua miili na wajeruhi waliomo.

Idadi ya raia wa mataifa mbalimbali waliopoteza maisha kwenye ajali ya ndege ya Ethiopia hadi sasa ni kama ifuatavyo; Kenya 32, Canada 18, Ethiopia 9, China 8, Italia 8, USA 8, Uingereza 7, Ufaransa 7, Misri 6, Uholanzi 5, Watano wenye hati za kusafiria za UN, Urusi 3, Morocco 2, Israeli 2, Ubelgiji 1,Uganda 1, Yemeni 1, Sudani 1, Togo 1, Msumbiji 1, Norway 1.

Taarifa kutoka  Shirika la ndege la Ethiopia

Habari Kubwa