PAC: TCCL ina madeni makubwa kushinda mtaji wake

21Oct 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
PAC: TCCL ina madeni makubwa kushinda mtaji wake

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imebaini kuwa Shirika la Mawasiliano nchini(TTCL) linaelemewa na madeni makubwa ya Sh.Bilioni 403 huku mtaji wake ni Sh.Bilioni 242.

Makamu Mwenyekiti wa PAC, Japhet Hasunga.

Kufuatia hali hiyo, PAC imetaka serikali kunusuru shirika hilo kwa kuliongezea mtaji au kuruhusu vyanzo vingine kwa TTCL ili kufanya kazi iliyokusudiwa.

Makamu Mwenyekiti wa PAC, Japhet Hasunga ameyasema hayo  mara baada ya kuhojiana na viongozi wa shirika hilo kufuatia hoja za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali za Mwaka 2019/20.

“Tumefanya uchambuzi wa hesabu zao imeonekana kwamba mtaji wao kwa ujumla ni Sh.Bilioni 242 wakati wa madeni ya Sh.Bilioni 403 kwa hiyo hicho ni kiashiria kwamba shirika haliendi vizuri,”amesema.

Pia, amesema soko halisi la TTCL halijakaa vizuri ikilinganishwa na washindani wengine.

Habari Kubwa