Padri anayetuhumiwa kubaka afunguliwa upya mashtaka

12Jan 2021
Daniel Sabuni
Hai
Nipashe
Padri anayetuhumiwa kubaka afunguliwa upya mashtaka

ALIYEKUWA Paroko wa Parokia ya Manushi Jimbo Katoliki la Moshi, Padri Erasmus Swai (44), ambaye anakabiliwa na kesi ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne, amefutiwa mashtaka ya awali na kufunguliwa upya.

Aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Manushi Jimbo Katoliki Moshi, Padre Erasmus Swai (kushoto), ambaye  ni mtuhumiwa wa kesi ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne, akitoka katika Mahakama ya Wilaya ya Hai akiwa na wakili wake, Moses Mahuna, baada ya kesi yake kuahirishwa jana. PICHA: DANIEL SABUNI

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nkamba Mbosela, jana, aliwasilisha hoja ya kuifuta kesi hiyo na kufunguliwa upya katika Mahakama ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Padri Swai, anadaiwa kutenda makosa hayo kwa mtoto mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi wa sekondari, mkoani Arusha.

Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama, Thurston Kombe, anayesikiliza kesi hiyo, Mbosela aliiambia mahakama kwamba upande wa mashtaka umebaini upungufu unaotokana na masuala ya kipelelezi.

Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa