Pambalu afurahishwa na ujenzi wa ofisi za Chama Jimbo la Makambako

18Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Njombe
Nipashe Jumapili
Pambalu afurahishwa na ujenzi wa ofisi za Chama Jimbo la Makambako

WANACHAMA wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mkoani Njombe wametakiwa kuendelea kushirikiana ili kukijenga chama hicho hasa katika kipindi hiki ambacho wanajenga ofisi ya chama hicho katika Jimbo la makambako.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Taifa, John Pambalu.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho wa Jimbo la Makambako Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Taifa, John Pambalu, amesema kuwa licha ya changamoto wanazokutana nazo kisiasa lakini bado wapo imara na amewataka wanachama hao kuendelea kuwa na umoja na ushirikiano ili kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo kwa wakati.

Aidha, Mwenyekiti huyo ameonesha kufurahishwa na kitendo cha wanachama wa Chadema jimboni hapo kuanza ujenzi wa ofisi kwa kuchangishana fedha zao wenyewe bila kutegemea wafadhili na Chama Taifa na kueleza kuwa kitendo hicho ni cha uzalendo na itakuwa funzo kubwa kwa wanachama wengine nchini.

“Mmeipa changamoto Wilaya nyingine nyingi zijifunze kutoka Makambako,na mnawajibu wale wanaosema Chadema hainaga ofisi, Chadema tuna ofisi mpaka za Wilaya zaidi kama ya Makambako”

 “Tanzania hakuna Chama chocote cha siasa kuanzia CCM mpaka vyote vilivyobaki isipokuwa Chadema peke yake ambacho wanaweza wakajenga ofisi za Chama kwa nguvu ya wanachama bila hata ya Ruzuku” amesema Pambalu.

Habari Kubwa