Pinda akumbusha amani kuelekea uchaguzi mkuu

22Oct 2020
Neema Hussein
KATAVI
Nipashe
Pinda akumbusha amani kuelekea uchaguzi mkuu

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewataka Watanzania kuitunza na kuilinda amani usiku na mchana kwani amani iliyopo ni tunu ya taifa.

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda akiwaombea kura wagombea wa CCM.

Kauli hiyo ameitoa leo katika Kata ya Kakese iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wakati akiwaombea kura mgombea wa nafasi ya ubunge Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi pamoja na wagombea wa nafasi za udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo amani ipo ya kutosha hivyo amesisitiza kuendelea kuitunza na kusema kuwa ilani ya CCM imeahidi kutoacha kuilinda amani hiyo.

"Bila amani tukianza kuvurugana hapa hakuna maendeleo, hakuna atakae lima, hakuna atakae tembea kwa uhuru,wapo watakaopata matatizo makubwa zaidi kuna wazee, watoto, walemavu na wakina mama wajawazito kwanini kwasababu amani imetoweka,"amesema 

 

Habari Kubwa