PM apongeza Watanzania kutosikiliza upotoshaji chanjo ya Uviko-19

22Oct 2021
Cynthia Mwilolezi
ARUSHA
Nipashe
PM apongeza Watanzania kutosikiliza upotoshaji chanjo ya Uviko-19

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewashukuru Watanzania kwa kutowasikiliza wapotoshaji kuhusu chanjo ya kujikinga na maambukizi ya Uviko-19 na kwenda kuchanja kwa wingi.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza  leo jijini Arusha katika mkutano wa tano wa  mwaka wa TEHAMA, Majaliwa amesema mpaka sasa kwa chanjo milioni moja zilizoletwa imefikia asilimia 96 ya watu waliochanja jambo ambalo linaleta faraja kuwa watu hawakubali kupotoshwa.

"Suala la afya ndugu zangu ni lako asije mtu asiye mtaalamu akakupotosha anayojua yeye,tuendelee kuwapuuza na tufuate maagizo ya wataalamu wetu wa afya kwa kuchukia hatua zote wanazotushauri na naomba tufuate kweli sababu bado ugonjwa upo japo idadi ya wagonjwa hospitalini imepungua,"amesema.

Amesisitiza watu kuendelea kuchukua tahadhali zote za kujikinga na maambukizi ili kupunguza maambukizi mapya na idadi ya vifo.

Amesema kwa nchi za watu waliochanja asilimia 90 kwa sasa hata wakikutana hawavai barakoa,ila kwa Tanzania kwa kuwa hawajafika hata asilimia 50 ya waliopata chanjo muhimu kuendelea kuvaa barakoa na kufuata pamoja na kuzingatia ushauri wote unaotolewa na wataalamu wa afya.

Habari Kubwa