Polepole awajia juu watumiaji wa mitandao

05Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Polepole awajia juu watumiaji wa mitandao

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewaonya watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kuweka habari za uongo zinazowahusu viongozi wa chama hicho tawala.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

Pia, kimesema Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally hana akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter.

Chama hicho tawala kimetoa taarifa yenye ufafanuzi huo leo Jumatano Desemba 5, 2018 ikiwa ni siku moja tangu Dk Bashiru Ally kuzungumza na Mwananchi na kukanusha taarifa za mtandaoni zilizomnukuu akimjibu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole inaeleza kuwa watu wanaotumia vibaya mitandao ya jamii wana lengo la kuleta taharuki.

“Kuna akaunti ya mtandao wa Twitter yenye jina la Bashiru Ally na inatoa kauli ambazo sio zake,” inaeleza taarifa hiyo.

Soma zaidi hapa chini;

Habari Kubwa