Polisi waionya Chadema ujio wa Lissu

25Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Polisi waionya Chadema ujio wa Lissu

Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo kali kwa viongozi wanaohamasisha mikusanyiko ya watu isiyo zingatia sheria za nchi na yenye lengo ovu kwa taifa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini (SACP) David Misime.

Kauli hii imetolewa leo Julai 25, 2020 baada ya kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaohamasisha watu kupitia mitandao ya kijamii kukusanyika kwenda kumpokea mmoja wa wanachama wao (taarifa haijamtaja) anayetarajia kuwasili nchini Tanzania Julai 27, 2020 kwa kutumia uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

Jeshi la polisi limesema linatambua Watanzani wapo kwenye kipindi cha maombolezo lakini hilo halitawazuia kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria wale wote wanaokusudia kufanya mikusanyiko bila kuzingatia sheria.

Taarifa kamili ya Polisi 

Habari Kubwa