Polisi Arusha waanza kutekeleza agizo la Gambo, Lema aonywa

17Feb 2020
Na Mwandishi Wetu
ARUSHA
Nipashe
Polisi Arusha waanza kutekeleza agizo la Gambo, Lema aonywa

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeanza kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyeagiza jeshi hilo kuwakamata na kuwahoji watu wanaosambaza video mitandaoni za ubovu wa barabara za kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana akizungumza na waandishi wa habari amemtaka Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kutoingilia suala hilo.

Tazama zaidi video hii

Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo alisema watu hao wanachafua taswira ya nchi na wana lengo baya kwani kulikuwa na njia sahihi kuliko kutumia mitandao ya kijamii, kitendo ambacho alikifananisha na Uhujumu Uchumi.

Gambo aliagiza Polisi kuwasaka, kuwakamata na kuwahoji waliotumia Mitandao ya Kijamii kuonesha ubovu wa miundombinu ya barabara ndani ya Mamlaka ya Hifadhi hiyo.

Tazama hapa chini agizo la RC Gambo kwa Kamanda wa Polisi Arusha 

 

Habari Kubwa