Polisi Kagera yashikilia viongozi sita wa Chadema

04Aug 2021
Lilian Lugakingira
Kagera
Nipashe
Polisi Kagera yashikilia viongozi sita wa Chadema

Jeshi la polisi mkoani Kagera linawashikilia viongozi sita wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), kwa tuhuma za kufanya mkutano uliolenga kuhatarisha amani.

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa walipata taarifa ya kufanyika kwa mkutano huo katika eneo la Kashai lililoko katika manispaa ya Bukoba leo na kwenda kuwakamata viongozi hao sita.

Kamanda huyo amesema kuwa majina ya wanachama hao wa Chadema wanaoshikiliwa kwa sasa yanahifadhiwa kutokana na uchunguzi kuendelea, huku akitoa onyo kali kwa wafuasi wengine wenye nia ya kufanya mikutano kama hiyo kuacha mara moja.

Habari Kubwa