Polisi Kitengo Maalumu kuwahudumia Watalii, Wanadiplomasia chaanzishwa

13May 2022
Na Mwandishi Wetu
Arusha
Nipashe
Polisi Kitengo Maalumu kuwahudumia Watalii, Wanadiplomasia chaanzishwa

​​​​​​​KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo, kwa niaba ya Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania amesema Polisi wameanzisha kitengo maalumu cha Utalii na Diplomasia ambacho kipo kwa ajili ya kuwahudumia Watalii na Wanadiplomasia wanaofika Tanzania,-

ACP Justine Masejo.

-hii ni baada ya Rais Samia kuzindua filamu ya Royal Tour.Kamanda Masejo amesema kwa Mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii nchini kumeanzishwa kituo cha Polisi maalumu kwa ajili ya kuhudumia Watalii na Wanadiplomasia ambapo Askari wake wamepatiwa mafunzo ndani na nje ya Nchi kuhusu namna bora ya kuhudumia watalii.Amesema kuwa kuna magari maalumu ambayo hutumiwa na kituo hicho kwa ajili ya doria mbalimbali ikiwemo kwenye vivutio vya utalii, hoteli za kitalii pamoja na maeneo mengine ambayo wageni hupenda kutembelea, mbali na hilo pia kuna vituo vidogo vya Polisi vilivyopo katika Wilaya ya Arumeru, Monduli, Longido na Karatu ambapo magari ya utalii hufika kwa ajili ya kupata taarifa za kitalii pamoja na ukaguzi wa usalama wa magari hayo.

Aidha, Kamanda huyo amesema Jeshi la Polisi litaendelea kumuunga mkono Rais Samia katika kuutangaza utalii kwa kuboresha mazingira ya kiusalama kwa Watalii

Habari Kubwa