Polisi Shinyanga wakamata silaha za kivita

21Nov 2022
Marco Maduhu
SHINYANGA
Nipashe
Polisi Shinyanga wakamata silaha za kivita

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga, limekata silaha mbili za kivita Ak47, ambazo zilikuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya uhalifu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionesha silaha ambazo wamezikamata na nyingine kusalimishwa na wananchi.

 

Jeshi hilo pia limepokea silaha 30 ambazo zimesalimishwa na wananchi kufuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camilius Wambura.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi, amebainisha hayo leo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Amesema Jeshi la Polisi kuanzia kipindi cha Septemba hadi Novemba mwaka huu kufuatia misako mbalimbali ambayo imeifanya imefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vya wizi, mdawa ya kulevya, mitambo ya kutengeneza pombe haramu, mitungi ya gesi, pamoja silaha mbili za kivita Ak47, huku silaha 30 zikisalimishwa.

“Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga tumekamata Silaha mbili za kivita AK47 ambazo zilikuwa zikitumika kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu, huku silaha 30 zikisalimishwa kufuatia agizo la IGP,”amesema Magomi.

“Tumekamata pia pikipiki 12, baiskeli moja zote za wizi, madawa ya kulevya aina ya Heroine kidonge kimoja, kete 10, bangi kilogram 55, mirungi kilogram 10, mitungi ya gesi mitano, Tv tatu, mitambo miwili ya kutengenezea Pombe haramu aina ya gongo,”ameongeza

Ametana vitu vingine walivyo vikamata kuwa ni majiko manne ya gesi, Kopyuta tatu, Sabwoofer sita, Monitor tatu, hadubini tatu za maabara, king’amuzi kimoja, magodoro matatu na bidhaa mbalimbali za dukani zikiwamo juice.

Aidha, Kamanda ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kufika katika Jeshi hilo wakiwa na nyaraka muhimu, ili kutambua vitu vyao ambavyo viliibiwa, huku akiwataka pia kuendelea kutoa taarifa za uhalifu.

Habari Kubwa