Polisi Simiyu waaswa kuepuka vitendo viovu

19Feb 2020
Happy Severine
Simiyu
Nipashe
Polisi Simiyu waaswa kuepuka vitendo viovu

Askari Polisi Mkoani Simiyu wameaswa kulinda hadhi ya jeshi hilo  kwa kujiepusha na vitendo viovu vinavyolitia dosari jeshi hilo. 

mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya askari polisi wa Wilaya ya Bariadi.

 

Rai hiyo imetolewa leo Februari 19,2020 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakati wa mazungumzo yake na jeshi hilo yaliyofanyika katika bwalo la polisi mjini Bariadi.

 

Mtaka amesema kuwa  baadhi ya vitendo hivyo  ni kutoa siri za jeshi, kuomba rushwa, utapeli na kushiriki kuharibu ushahidi katika baadhi ya kesi.

“Ni jambo la aibu kwa askari kushiriki katika uhalifu, kutoa siri za jeshi na kugeuka kuwa mtoa taarifa kwa wahalifu...mnatakiwa muipende  kazi yenu na  kuepuka mambo yanayodhalilisha jeshi na badala yake mlinde na kujenga heshima ya jeshi letu ,” amesema Mtaka.

Baadhi ya askari polisi wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayuko lichani) walipotembelewa na mkuu hiyo.

 

Habari Kubwa