Polisi washtumiwa kukwamisha kesi za udhalilishaji 

16Jan 2019
Rahma Suleiman
ZANZIBAR
Nipashe
Polisi washtumiwa kukwamisha kesi za udhalilishaji 

Mkuu wa wilaya ya kusini Unguja Idrisa Kitwana amesema kuwa baadhi ya askari polisi katika kituo cha polisi Makunduchi wamekuwa wakikwamisha kesi za udhalilishaji. 

Mkuu wa wilaya ya kusini Unguja Idrisa Kitwana akizungumza katika kikao na kamati ya maendeleo, Italii,habari na wanawake ya baraza la wawakilishi.

Amesema baadhi ya askari wa jeshi hilo wamekuwa wakisuluhisha kesi hizo na kushindwa kusonga mbele katika upatikanaji wa haki. 

Mkuu wa wilaya huyo aliyaeleza hayo wakati akizungumza katika kikao na kamati ya maendeleo, habari, utalii na wanawake walipofika ofisi za mkuu wa mkoa kusini Unguja. 

Amesema baadhi ya askari hao wamekuwa ndio kichocheo cha kusuluhisha kesi hizo na hatimae kufungisha ndoa kwa mtuhumiwa wa kesi za udhalilishaji na wahanga wa matukio hayo.

Habari Kubwa