Prof. Lipumba apata chanjo ya corona

22Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Prof. Lipumba apata chanjo ya corona

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepata chanjo ya kwanza ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

Profesa Lipumba amepata chanjo hiyo leo Jumatano Julai 22,2021 katika kliniki ya Umoja wa Mataifa zilizopo Masaki.

Akizungumza na waandishi baada ya kutoka kupata chanjo hiyo amesema amejikuta akipata nafasi hiyo kupitia mke wake, Gojina Mtenga, anayefanya kazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto Duniani (Unicef), Cox Bazaar nchini Bangladesh.

"Kama mlivyosikia wenzetu wa mashirika haya ya kimataifa wameruhusiwa kuanza kupata chanjo hizi pamoja na familia zao.

"Mimi kupitia mke wangu ndio imeniwezesha leo kuja kupata chanjo hii na nilipata taarifa usiku wa jana ikinitaka nifike hapa leo saa tano asubuhi nashukuru kwa kulikamisha hili, "amesema Profesa Lipumba.

Hata hivyo amesema baada ya chanjo hiyo  ya awali anatakiwa arudi tena baada ya wiki sita mpaka nane kupata chanjo ya pili ili kukamilisha chanjo nzima ya kujikinga ya kujikinga na ugonjwa huo.

Habari Kubwa