Prof. Lipumba atinga ngome ya Maalim Seif Zanzibar

16Aug 2018
Rahma Suleiman
ZANZIBAR
Nipashe
Prof. Lipumba atinga ngome ya Maalim Seif Zanzibar

Kwa mara ya kwanza Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba amezungumza na wafuasi wa CUF kisiwani Unguja tangu chama hicho kuwa na mgogoro. 

Profesa Ibrahim Lipumba.

Mgogoro huo ambao umedumu kwa  muda wa miaka miwili sasa na kupelekea wafuasi wa chama hicho kugawika pande mbili ambapo upande mmoja unamunga mkono katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na wengine wanaomuunga mkono Mwenyekiti Profesa Lipumba. 

Akizungumza katika mkutano ambao haukuungwa mkono na wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Maalim Seif, Profesa Lipumba amesema kuwa hakuna wa kiongozi  wa CUF alieshiriki kutetea haki ya wazanzibar kuliko yeye.

Amesema mwaka 2001 alipigwa na kuumizwa kwa kudai haki ya wazanzibari kwa kupinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2000.

"Nilipigwa na kuvunjwa mkono wangu kutokana na kuwahamasisha wananchi maandamano ya amani ya kudai matokeo halali ya uchaguzi wa 2000 na kudai katiba ya Tanzania "amesema. 

Alieleza kuwa katika wanasiasa wa Tanzania yeye ndie kiongozi pekee aliyemstari wa mbele kupigania haki na  maslahi ya wazanzibari ndani ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Habari Kubwa