Prof. Lipumba awaahidi wakulima wa Tumbaku kuuza China

15Sep 2020
Boniface Gideon
TABORA
Nipashe
Prof. Lipumba awaahidi wakulima wa Tumbaku kuuza China

Mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amesema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha anasimamia na kuwatafutia masoko ya Kimataifa wakulima wa zao la Tumbaku hususani Nchi ya China kwa kuwa Taifa hilo linaongoza Duniani  kwa watumiaji wengi wa zao hilo.

Mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Prof. Ibrahim Lipumba

Mgombea  Urais kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha anasimamia  na kuwatafutia  Masoko ya Kimataifa wakulima wa zao la  Tumbaku  hususani  Nchi  ya  China   kwakuwa  Taifa Hilo linaongoza   Duniani  kwakuwa  na Watumiaji  Wengi  wa   zao hilo  ambapo  Nchi  hiyo  inazaidi Watumiaji  milion 400   wanavuta tumbaku.

Akizungumza   leo Septemba  15 na  wananchi katika Viwanja  vya  Igalula Station kata ya Igalula wilayani Uyuwi mkoani Tabora,  Prof. Lipumba amesema China ina zaidi ya watumiaji wa Tumbaku milioni 400.

Amesema mkoa huo unasifika kwa kulima zao la Tumbaku lakini wakulima wake wamesahulika   kwa kutopewa kipaumbele kikubwa hali iliyowafanya kuendelea kuwa masikini baada  yakushindwa  kutafuta  masoko makubwa ya kimataifa  ambayo yanaushindani mkubwa wa bei.

Prof.Lipumba amesema wakulima wanahitaji  kupata  Serikali itakayosimamia maendeleo ya uchumi na itakayowekeza kwenye sekta ya kilimo kwa kujenga mazingira mazuri ya biashara ili viwanda vya Tumbaku viendelee kuwepo pamoja na kukuza soko lake.

Habari Kubwa