Prof.Lipumba awaombea ruhusa wagombea walioshinda rufaa

16Sep 2020
Boniface Gideon
TABORA 
Nipashe
Prof.Lipumba awaombea ruhusa wagombea walioshinda rufaa

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba ameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwaruhusu wagombea wao walioshinda Rufaa waruhusiwe kuanza kampeni kwa kuwa siku zinazidi  kwenda.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba.

Amesema NEC inapaswa kutenda haki kwa kupeleka barua kwa wagombea wao waliokata rufaa na zikakubaliwa kwani tayari kampeni zimekwishaanza zaidi ya siku  20 sasa.

Kauli hiyo  ameitoa  leo Septemba 16,2020 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bukene Wilaya ya Nzega mkoani Tabora kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Amesema anashangaa kuona mpaka sasa wagombea wao hawajapewa barua na ikiwa tayari tume imeshajiridhisha na kuwarejesha lakini changamoto ni ukosefu wa barua rasmi.

Habari Kubwa