Prof.Lipumba ateua 13 kuongeza nguvu CUF

28Apr 2019
Mary Geofrey
Dar es salaam
Nipashe Jumapili
Prof.Lipumba ateua 13 kuongeza nguvu CUF

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimewateuwa wanachama 13 kushika nafasi mbalimbali za uongozi ili kusaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, aliwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa, wameteua wanachama ambao miongoni mwao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

Aliwataja walioteuliwa kuwa ni Zaynab Amir Mndolwa Mkurugenzi wa Fedha,l na Omary Mohamed Omary ambaye atakuwa Naibu Mkurugenzi.

Wengine walioteuliwa ni Mohamed Habibu Mnyaa, atakayekuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge na Sera na Mohamed Ngulangwa atakayekuwa Naibu Mkurugenzi na Mneke Jafar Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi na Mohamed Vuai Makame atakayekuwa Naibu Mkurugenzi.

Prof. Lipumba alisema wengine ni Abdul Juma Kambaya Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma na Mbarouk Seif Salim Naibu Mkurugenzi.

Alisema kuwa Haroub Mohamed Shamis kuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Salvatory Magafu kuwa Naibu Mkurugenzi.

Wanachama wengine walioteuliwa ni Thinney Juma Mohammed kuwa Mkurugenzi wa Mafunzo na Uhamasishaji na Masoud Omary Mhina kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mafunzo na Uhamasishaji na Yusuph Mohamed Mbugiro aliyeteuliwa kuwa Ofisa Tawala wa Ofisi Kuu ya Dar es Salaam.

Kashalika Prof. Lipumba ameteuwa viongozi wa Jumuiya ya Vijana wa (CUF- JUVCUF)pamoja na Jumuiya ya Wanawake (JUKECUF)

Hata hivyo alisema kwa upande wa JUVCUF Kaimu Mwenyekiti ni Hamidu Bobali, Kaimu Makamo Mwenyekiti Faki Suleiman Khatib, Kaimu Katibu Mtendaji, Yusuph Kaiza Makame pamoja na Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Mbaraka Ismaili Chilumba.

Pia alisema JUKECUF Kaimu Mwenyekiti, Dhifaa Mohamed Bakar, Kaimu Makamo Mwenyekiti, Kiza Husein Mayeye, Kaimu Katibu Mtendaji Anna Ryoba Paul pamoja na Kaimu Naibu Katibu Mtendaji Leila Jabir Haji.

“Uteuzi huu umefanywa na Mwenyekiti wa CUF kwa kushauriana na Makamu Mwenyekiti na uteuzi huu utafikishwa mbele ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa kuthibitishwa," alisema Prof. Lipumba

Habari Kubwa