Qnet yaadhimisha Siku ya Mazingira duniani na maji safi vijijini

06Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Qnet yaadhimisha Siku ya Mazingira duniani na maji safi vijijini

Kila mwaka, Juni 5 ni Siku ya Mazingira Duniani, katika kusherehekea mwaka huu, kampuni ya QNET ikishirikiana na Shirika la Water for Africa (WFA), inaazimisha mwaka wa sita wa mradi wa maji mkoani Iringa Tanzania.

WFA ilianzishwa mwaka 2015 na Julie na  Phil Hepworth kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa Iringa kwa kuchimba visima.

Uchimbaji wa kila kisima unagarimu takribani USD 5,000 na kila kisima kinahudumia zaidi ya wanakijiji 3,000.

Kisima cha kwanza kilichimbwa kijijini Mtwango, Wilayani Mufindi. Hadi kufikia mwaka jana, WFA ikishirikiana na QNET wamechimba visima zaidi ya 45 vinavyo hudumia watu zaidi ya milioni mbili.

Ushirikiano huu, ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira kuu ya kampuni ya QNET, kuwa kampuni endelevu inayo  tunza na kuhifadhi rasilimali.

"Tunajitahidi kuwa kampuni endelevu kwa kutunza rasilimali kwa ajili ya vizazi vijavyo," alisema Malou Caluza, Mkurugenzi wa QNET.

"Tunataka kuacha kumbukumbu chanya kwa kuhakikisha tunafanyakazi na kampuni ambazo zina tunza mazingira katika matumizi ya rasilimali," aliongeza.

Katika jitihada hizi, WFA na QNET wameungana na RYTHM Tanzania na kuanzisha shamba la maparachichi pamoja na karanga za makademia.

Shamba hili la hekari 50 lipo Mkoani Iringa na linatoa ajira kwa wanakijiji. Mapato yanayotokana na mavuno ya shamba hilo yanatumika kuchimba visima zaidi na kuvikarabati.

Shamba hili linasimamiwa chini ya mradi uitwao Footprint Project. Mradi huu unahakikisha kuwa uchimbaji wa visima mkoani huko unakua endelevu.

Zaidi ya hapo, kwa kuwezesha upatikanaji wa maji, mradi huu unahakikisha wasichana wanapata nafasi ya kuhudhuria shule badala ya kutumia masaa mengi kuchota maji.

Akizungumzia mradi huu, Mkurugenzi wa mradi huo bwana James Raj alisema; “Kabla ya mradi huu wanawake walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita 11 kutafuta maji ambayo mara nyingi huwa sio safi.”

“Kabla ya mradi huu, wanakijiji walikua wanatumia maji  kutoka katika mabwawa na mito wanapo nyweshea mifugo yao, maji hayo yalikua ni machafu na sio salama kwa afya,” alisema.

"Kupitia shamba hili, tunahakikisha mradi wa uchimbaji wa visima unakua endelevu na unajitegemea bila ya kuhitaji msaada wa nje," aliongeza

Habari Kubwa