Rage awaonya wanaopotosha chanjo corona

04Aug 2021
Halima Ikunji
Tabora
Nipashe
Rage awaonya wanaopotosha chanjo corona

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa wa Tabora kupitia CCM, Ismail Aden Rage, amewataka baadhi ya wananchi kuacha tabia ya kuzuia watu wasiende  kupata chanjo ya UVIKO 19 katika vituo vilivyopangwa na serikali.

Rage akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake leo baada ya kumaliza uzinduzi wa chanjo ya UVIKO 19 katika ukumbi wa Mtemi Mwanakiyungi Mkoani Tabora.

Amesema kwamba wasifanye kampeni hiyo ili kuichafua serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan hawatafaidika na kitu chochote.

Amsema kama kuna baadhi ya watu wanafanya mtindo huo waache mara moja kwasababu serikali imejipanga kwa kuhakikisha imawashughulikia ipasavyo.

Amesema kwamba mtindo huo ni mbaya na unaweza ukamuingiza pabaya na chanjo ni hiari ya mtu mwenyewe na siyo kuwazuia wengine wenye nia ya dhati katika kupata chanjo hiyo.

"Natoa mfano huu Juni 1 mwaka huu nilikuwa Taranta Marekani nilichanja hiyo kinga na sijadhurika chochota mpaka sasa nina miezi miwili sijapata madhara yeyote," amesema

Hata hivyo Rage amesema kwamba dawa hizo ni sahihi na madai ya watu wakisema zimetayarishwa kwa muda mfupi siyo kweli.

Amesema Lazima watu wanatakiwa kuelewa watu wenye fedha yao duniani kuwa nchi za Magharibi ndio matajiri wakubwa duniani.

Amesema ilitumika fedha nyingi kwenye utafiti kuliko wakati mwingine wowote, Lakini kwenye hali kama hii ni lazima dawa zipatikane mapema.

Habari Kubwa