Rais Magufuli amteua Mnadhimu Mkuu JWTZ

14Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Rais Magufuli amteua Mnadhimu Mkuu JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Februari, 2018 amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ).

rais john magufuli.

Mbali na uteuzi huo, Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wafuatao;

1. Brig Jen. J.G. Kingu

2. Brig Jen. M.S. Busungu

3. Brig Jen. R.R. Mrangira

4. Brig Jen. B.K. Masanja

5. Brig Jen. G.T. Msongole

6. Brig Jen. A.F. Kapinga

7. Brig Jen. K.P. Njelekela

8. Brig Jen. A.S. Bahati

9. Brig Jen. M.E. Mkingule

10. Brig Jen. S.S. Makona

Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ataapishwa kesho tarehe 15 Februari, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

Habari Kubwa