Rais Samia amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu TPA

28Mar 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe Jumapili
Rais Samia amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu TPA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, ili kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha bandarini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Samia ametoa uamuzi huo leo Jumapili, Machi 28, 2021 baada ya kusikiliza ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma na kugundua mapungufu katika idara yake.

“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,” amesema Rais Samia.

 

Habari Kubwa