Rais akataa kung'atuka madarakani

14Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Rais akataa kung'atuka madarakani

Rais wa kike pekee barani Afrika, Rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim amekataa kuachia ngazi kufuatia kashfa ya matumizi mabaya ya fedha, siku moja baada ya kutangazwa kwamba atang'atuka madarkani.

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Rais wa Mauritius Dk.Ameenah Gurib-Fakim wakati alipofanya ziara nchini Tanzania mwaka jana.

Bi Gurib-Fakim amekanusha madai kwamba alitumia maelfu ya dola kwa matumizi binafsi kwa kutumia kadi ya benki ya shirika la msaada.

Ofisi yake imesema matumizi hayo yalikuwa bahati mbaya na fedha zimerudishwa.

Waziri mkuu wa nchi hiyo alisema angejiuzulu siku ya Jumatatu.

Lakini ofisi ya Rais imekanusha taarifa hizo.

"Mheshimiwa Ameenah Gurib-Fakim, hana hatia yoyote na ametoa ushahidi wakutosha hivyo amekataa wazo lolote la kuachia madaraka." taarifa kutoka ofisi ya rais imesema.

Taarifa hiyo imeongeza pia kwamba Gurib-Fakim, ambaye ni mwanasayansi maarufu, ' alikuwa na kadi iliyofanana kutoka benki sawa na hiyo iliyotumiwa na shirika la misaada na kwa bahati mbaya akaitumia kununua vitu binafsi'

Ofisi yake imesema dola za kimarekani 27,000 zimerudishwa na Bi Gurib-Fakim atachukua' hatua za kujitetea kisheria'

Chanzo: BBC Swahili

 

Habari Kubwa