Rais atunuku nishani 43 kwa viongozi

12Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Rais atunuku nishani 43 kwa viongozi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein ametunuku nishani 43 zilizotukuka kwa viongozi na watumishi wa umma katika maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dkt. Shein ametoa nishani hizo kwa mtu ambae aliasisi, alishiriki na kutukuza pamoja na kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea mwaka 1964.

Pamoja na hayo Dk. Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili kuwa chachu ya kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa uwekezaji miradi mikubwa ya maendeleo visiwani .

Katika maadhimisho hayo mbali ya nishani hizo serikali ya Zanzibar huzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni ishara ya ukombozi wa fikra na maendeleo ya kiuchumi ya taifa hilo.