Rais Magufuli awapongeza wanawake

08Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Rais Magufuli awapongeza wanawake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 8, 2018 katika siku ya wanawake duniani amewapongeza wanawake wote wa Tanzania na kuwatakia kheri katika siku yao hii muhimu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Magufuli ametoa ujumbe huo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kuwa wanawake wamekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii na kusema daima ataendelea kuwaheshimu 

"Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu" alisema Rais Magufuli.