Rais Samia aahidi kuboresha mazingira, maslahi kwa Wauguzi

12May 2021
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
Rais Samia aahidi kuboresha mazingira, maslahi kwa Wauguzi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuboresha mazingira ya kazi na maslahi kwa Wauguzi wote nchini ili waweze kutimiza majukumu yao vizuri na kwa usalama zaidi.

Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia ametoa ahadi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter na Instagram kwa kuwa leo ni siku ya maadhimisho ya Wauguzi Dunia.

“Nawatakia kheri Wauguzi wote katika kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani. Serikali inatambua na kuthamini mchango wenu katika jamii. Nawaahidi kuwa kutaendelea kuboresha mazingira na maslahi yenu ya kazi ili mtimize majukumu yenu vizuri na kwa usalama. Chapeni kazi, tunawategemea” ameandika Rais Samia.

Habari Kubwa