Taarifa iliyotolewa leo Mei 14,2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus inasema mapendekezo hayo ni mwendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichokifanya hivi karibuni mkoani Dodoma na kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu kuhusu ongezeko la mishahara.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh9.7 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.