Rais Samia afanya teuzi za viongozi

30May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe Jumapili
Rais Samia afanya teuzi za viongozi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa mikoa 11, huku makatibu tawala tisa akiwabadilisha vituo vya kazi na wengine sita wakibaki katika vituo vyao vya kazi.

Samia Suluhu Hassan.

Sambamba na uteuzi huo, Pia Rais Samia amefanya uteuzi wa watendaji wawili wa Mashirika ya Umma ambapo amemteua William Erio kuwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC) huku Dk John Mduma kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Kutokana na taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, jana Mei 29, Rais Samia amewateua baadhi ya viongozi waliokuwa kwenye chama na wengine waliokuwa serikalini wakitumikia katika nafasi nyingine.

Baadhi ya walioteuliwa ni pamoja na Rodrick Mpogolo ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. Kabla ya uteuzi huo, Mpogolo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara.

Rais Samia amemteua Ngusa Samike kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Kabla ya uteuzi huo, Samike alikuwa Katibu wa Rais, Hayati John Magufuli.

Hata hivyo, Rais Samia amemteua Athuman Kihamia kuwa katibu tawala wa Mkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huo, Kihamia alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Habari Kubwa