Rais Samia afuta mashamba 11 na kufufua 49 Kilosa

07Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Morogoro
Nipashe
Rais Samia afuta mashamba 11 na kufufua 49 Kilosa

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefufua mashamba 49 yenye hekari 45,788.5 baada ya kufuta mashamba 11 yenye hekari 24, 119 katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Mbali na kufuta na kufufua mashamba hayo, pia imeundwa timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi na wataalamu wa mikoa na wilaya ili kufanya uhakiki na kupanga matumizi bora ya ardhi yatakayosaidia wananchi.

Maamuzi hayo ya Rais Samia yamewasilishwa na Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, leo Juni 7, 2021 katika kikao alichoketi pamoja na Watendaji, Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwenye ziara yake ya siku moja mkoani humo.

Habari Kubwa