Rais Samia atarajia kuzungumza na Wanawake 10,000 Dodoma

06Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe Jumapili
Rais Samia atarajia kuzungumza na Wanawake 10,000 Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuzungumza na wanawake zaidi ya 10,000 jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa Leo Juni 6, 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.

Mtaka amesema Rais Samia atazungumza na wanawake wa Mkoa huo kwa niaba ya wanawake wote nchini katika ukumbi wa Jakaya Convertion, siku ya Jumanne tarehe 8 Juni, 2021.

Amesema wanawake kwa uwakilishi wao wa makundi kutoka katika Wilaya za Dodoma na maeneo ya karibu wamepewa mwaliko wa kushiriki katika mkutano huo.

"Kwa uchache pia kama makundi ya wabunge wanawake bila kujali uko chama gani, madiwani na makundi kama wajasiriamali, mama ntilie na kila aina ya wanawake watapata nafasi ya kuwakilishwa na wenzao," amesema RC Mtaka.

Habari Kubwa