Rais Samia atarajiwa kufanya ziara ya siku mbili Arusha

14Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Arusha
Nipashe
Rais Samia atarajiwa kufanya ziara ya siku mbili Arusha

RAIS Samia Suluhu Hasani, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Arusha, ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, leo Oktoba 14, 2021 Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, amesema Rais atawasili mkoani humo Oktoba 16.

Amesema akiwa mkoani humo, atatembelea mradi wa maji wenye  thamani ya shilingi bilioni 520 uliopo Chekereni wilayani Arumeru, pamoja na kuzindua mradi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Engutoto unaojengwa na fedha za ndani za Halmashauri ya jiji la Arusha.

"Baada ya uzinduzi huo Rais Samia anatarajia kuhutubia wananchi katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid" amesema Mkuu huo wa Mkoa.

Aidha, Mongela amesema Oktoba 18, Rais atazindua Kiwanda cha Nyama Elia Food Overseas LTD kilichopo Namanga wilayani Longido, atazindua mradi wa maji wilayani hapo pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Habari Kubwa