Rais Samia kuapisha viongozi tarehe 17,19

16May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Rais Samia kuapisha viongozi tarehe 17,19

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwaapisha Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Taasisi walioteuliwa, siku ya Jumatano Mei 19, 2021 majira ya saa 4 :00 asubuhi badala ya Jumanne kama ambavyo ilivyokuwa imetangazwa hapo awali.

Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Rais Samia atawaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani na Majaji wa Mahakama Kuu siku ya Jumatatu tarehe 17 Mei, 2021 kuanzia saa 9:00 Alasiri.

Viongozi hao wataapishwa katika ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam na matukio yote yatarushwa mubashara kupitia vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao ikiwemo youtube channel ya Ikulu Mawasiliano na kurasa rasmi za Ikulu Mawasiliano katika Instagram, Twitter na Facebook.

Habari Kubwa