RC ahamasisha Watanzania kutembelea Hifadhi ya Katavi

14Jun 2019
Mary Geofrey
KATAVI
Nipashe
RC ahamasisha Watanzania kutembelea Hifadhi ya Katavi

MKUU wa Mkoa wa Katavi,Juma Homera, amewataka Watanzania  kujijengea utamaduni wa kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea hifadhi mbalimbali za taifa zilizopo nchini hususani Hifadhi ya Katavi.

MKUU wa Mkoa wa Katavi,Juma Homera

Homera ametoa wito huo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari, waliotembelea hifadhi hiyo kwa lengo la kujienoa vivutio vilivyopo katika mkoa huo.

Amewahamisha Watanzania kutembelea vivutio  vya Hifadhi ya Taifa ya Katavi na fukwe za Ziwa Tanganyika na kuwekeza kibiashara.

"Nitoe wito kwa Watanzania na watu mbalimbali kuja kutembelea vivutio vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kujionea aina mbalimbali za wanyama wanaopatikana katika mbuga hii  wakiwamo Twiga weupe ambao hupatikana katika hifadhi hii pekee," amesema Homera.

Amesema mkoa wa huo una fursa nyingi ikiwamo uchimbaji wa madini hivyo kuwakaribisha wawekezaji wa madini kufika kuwekeza.

Habari Kubwa