RC aagiza mali zitaifishwe

02Aug 2017
Frank Monyo
Nipashe
RC aagiza mali zitaifishwe

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi ametoa mwezi mmoja mali za watendaji 21 wa vijiji katika halmashauri ya Wilaya ya Manyoni zitaifishwe na kuuzwa ili kufidia fedha walizotumia za chakula cha njaa katika kipindi cha mwaka 2012.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo katika baraza maalumu la madiwani la kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali ambapo kulikuwa na hoja ya watendaji wa vijiji 30 waliokusanya kwa wananchi shilingi milioni 15 kwa ajili ya chakula cha njaa na hawakuziwasilisha katika halmashauri hiyo.

Amesema kitendo hicho ni wizi na hakistahili kuvumiliwa licha ya watendaji tisa kurejesha kiasi cha shilingi milioni 3 na hivyo kusalia watendaji 21 wanaodaiwa shilingi 11,991,700 walizokusanya.

"Huu ni wizi na hatutauvumilia, hao watendaji wa vijiji hakikisheni wanarudisha fedha za serikali, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, anzisheni utaratibu wa mahakama tembezi muwafuate huko waliko, kamateni mbuzi, kuku, uzeni tupate hiyo fedha na zoezi hilo lifanyike ndani ya mwezi wa nane (Agosti)," ameagiza Dkt Nchimbi.

Habari Kubwa