RC akwama siku mbili kukifikia kijiji

01Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
RUKWA
Nipashe
RC akwama siku mbili kukifikia kijiji

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh.Joachim Wangabo amelazimika kuacha gari lake na kutembea kwa mguu ili kukifikia moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya Kalambo mkoani humo kutokana na miundombinu mibovu ya barabara.

Gari waliopanda wataalamu kutoka Ofisi ya mkoa wa Rukwa likiwa limekwama huku wataalamu hao kwa ushirikiano na wajumbe wa Kamati ya ulinzi ya Mkoa wakijaribu kulikwamua kutoka kwenye tope zito wakati wakitokea kijiji cha Jengeni Kata ya Kitete, Wilayani Kalambo.

Hali hiyo imetokea wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea kijiji cha Nondo, Kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo kwaajili ya kukutana na wananchi hao na kufahamu changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo. 

Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa mkoa aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na wataalamu kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akivushwa katika daraja la miti na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nondo Robert Sikombe kuelekea katika kitongoji cha Kamleshe ili kukutana na wananchi hao na kufahamu changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo. 

Msafara huo ulikwama kwenye tope zito lililosababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha hali ya barabara kuwa mbaya. 

Gari waliopanda wataalamu kutoka Ofisi ya mkoa wa Rukwa likiwa limekwama huku wataalamu hao kwa ushirikiano na wajumbe wa Kamati ya ulinzi ya Mkoa wakijaribu kulikwamua kutoka kwenye tope zito wakati wakitokea kijiji cha Jengeni Kata ya Kitete, Wilayani Kalambo. 

Hali hiyo ilipelekea Mkuu wa Mkoa na msafara wake kutembea kwa mguu kwa takribani saa moja na nusu kufika katika kijiji hicho, ambapo walivuka madaraja mbalimbali ya miti ambayo yana usalama mdogo kwa wananchi wa vijiji vinavyotumia barabara hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akivuka daraja la miti katika mto china ili kufika katika kijiji cha Jengeni na kuelekea katika kitongoni cha Kamleshe, kijiji cha Nondo, Kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo. 

Habari Kubwa