RC Andengenye awapongeza wanahabari kutoa elimu corona

14Oct 2021
Pendo Thomas
KIGOMA
Nipashe
RC Andengenye awapongeza wanahabari kutoa elimu corona

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye amepongeza waandishi wa habari mkoani humo katika mchango na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa corona.

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiwa katika mdahalo wa  uhuru wa kujieleza, maadili ya uandishi wa habari, pamoja na kumuenzi Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere uliohusisha waandishi wa habari na viongozi wa serikali mkoani humo.

Andengenye, amesema waandishi wa habari wameendelea kuwa mstari wa mbele kueleza hatua mbalimbali za kujikinga na uhamasishaji wa  wananchi kupata chanjo.

"Nichukue nafasi hii kwa dhati ya moyo wangu kutambua mchango wa waandishi wa habari katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona" amesema Andengenye.

Prosper Kwigize, mwandishi wa habari amesema ili kujenga imani kwa wananchi kukubali matumizi ya chanjo serikali inapaswa kutumia zaidi waandishi wa habari kufikisha elimu.

Ameeleza baadhi ya wanajamii wana mitazamo hasi juu ya suala hilo hivyo endapo vyombo vya habari vitaendelea kutoa elimu itasaidia kuongeza mwamko wa watu kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19.

Habari Kubwa