RC Byakanwa awataka wenye dawa asili za magonjwa ya hewa wajitokeze

23Feb 2021
Dotto Lameck
Mtwara
Nipashe
RC Byakanwa awataka wenye dawa asili za magonjwa ya hewa wajitokeze

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amewataka wote wenye dawa zinazohusiana na mfumo wa hewa wajitokeze kwa wingi katika ofisi yake ili waelekezwe jinsi zinavyofanya kazi na baadaye kusajiliwa ili ziwasaidie Watanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa.

“Nawataka wote ambao wana tiba za asili za pumu, kifua, mafua, maumivu ya mwili na dawa zozote zinazohusiana na mfumo wa hewa, wajitokeze, waje Ofisini kwangu watueleze dawa zao zinavyofanya kazi na tutawapa utaratibu wa kuzisajili ili ziwasaidie Watanzania,” RC Byakanwa.

RC Byakanwa ameongeza kuwa hata kauli aliyoitoa Rais Magufuli kuhusiana na barakoa kutoka nje alimaanisha kwanini tusipate majibu kutoka kwetu.

“Rais Magufuli alivyosema mambo ya barakoa alikuwa anatupeleka kule kwamba kwanini tusipate majibu kutoka kwetu, sisi kule kwetu Bukoba, kuna dawa Watu wanajua mjamzito anameza dawa gani ya asili, aliyevunjika au anayekohoa wameze dawa gani, hawa ndio nawataka waje ili dawa zao zisajiliwe.” RC Byakanwa.

Habari Kubwa