RC Chalamila azindua kituo cha afya Mbeya

20Nov 2019
Kelvin Innocent
Mbeya
Nipashe
RC Chalamila azindua kituo cha afya Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, amewapongeza viongozi wa mkoa huo kwa utendaji ambao unaridhisha.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, PICHA MTANDAO

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kituo cha afya cha kata ya Isongole na kutoa pongezi kwa wasaidizi wake waliofanikisha zoezi la ujenzi wa hospitali hiyo.

Chalamila amesema licha ya hospitali hiyo kuaanza kutoa huduma za matibabu kwa wananchi, bado haijakamilika kuwa na vifaa tiba vyote ambavyo ni muhimu inayaotakiwa kuwa navyo.

“Nimeshamwambia Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya waniandikie mchanganuo wote wa vifaa halafu tuupeleke kwa wadau na naamini watatupatia hivyo vifaa muda si mrefu,” amesema Chalamila.

Kwa upande mwingine, Chalamila amewapongeza viongozi wa kata hiyo kwa kupita bila ya kupingwa kutokana na wananchi kuona maendeleo yakizidi kukua kwa kasi.

Aidha, Chalamila ametumia ufunguzi huo kama njia ya kuhamasisha wananchi wa kata hiyo kujitokeza katika uchaguzi ujao.

Hata hivyo, amesema hakuna haja kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuingia katika uchaguzi kwa sababu maendeleo yanajionesha yenyewe na wananchi wanaona jinsi yanavyoendele bila mtu kuonewa.

“CCM kirefu chake ni Chama Cha Mapinduzi na ACT?, semeni. Wewe unaleta maneno ya kiingereza kwa mtu wa Isongole kuna mtu atakuelewa, hakuna haja ya kuingia kwenye uchaguzi ni kupita tu na nawaombea Mungu na mwaka 2020, waliogoma wakagome na kwenye ubunge,” amesema Chalamila.

Chalamila amesema wanaogoma kwa sababu hawachaguliwi na wananchi wenyewe, amewaita ni ‘wahuni na waongo’ na anasubiri mwakani wagome tena.

Habari Kubwa